Angola
Algeria
Benin
Botswana
Cameroon
Cabo Verde
Congo
Gambia
Ghana
Guinee
Ivory Coast
Kenya
Liberia
Madagascar
Malawi
Mali
Mozambique
Namibia
Nigeria
Rwanda
Senegal
South Africa
Swaziland
Tanzania
Togo
Uganda
Zambia
Zimbabwe



HU Squad - Hardcore Unity: Rap si mchezo!



Group la Hardcore Unity limekuwa formed na artists ambapo kutokana na makundi mawili yaani Mad Group lililokuwa na Jacob Makalla a.k.a. JCB, Manongi, na Nigga Nyange. Wakati lile kundi la Flava Dogz, liliundwa na Space Malic na Lord Izz ambao kwa pamoja waliform 'Hardcore Unity'. Wakati huo ilikuwa ni mwezi june 1997, ambapo tuliweza kutoa kibao kilichojulikana kama 'Rap si mchezo' kilichotengenezwa na Jumanne (Thomas) wa Netherlands.
Wimbo huu tuliimba ni: JCB, Spac & YZ wa Achongpong Clan.

Hardcore Unity aka HU Squad wanasema kitu kilichowavutia hadi kuingia katika fani ya hiphop ni kutokana na kuvutiwa na kundi la Das EFX la nchini Marekani, katika albam yao ya 'Dead field'. Albam hiyo ilitupa msisimko mkubwa wa kuungana na kuweza kutoa single nne ambazo zinapigwa redio station mbalimbali mchini. Vile vile wanazo nyimbo kadhaa zakuweza kutosha kutoa albam.

Jacob amezitaja na kueleza kuhusu single zao kuwa ni: 'Rap si mchezo' ambao unagusia kwamba muziki wa rap si wa kudharauliwa kwani unaweza kukusaidia ukawa na maisha mazuri baadae. Vile-vile 'Brain surgery' umemlenga Mtanzania wa kawaida ambaye anajishughulisha kupata maisha mazuri hapo baadae.

Akizungumzia kuhusu artist mwenzao Maffiola Attoh ambaye sauti yake inafanana na ile ya Lauren Hill wa Marekani kuwa ameolewa na Mjamaica aliyetambulika kama Attoh Kidanu ambaye ni mfanya biashara mkoani Arusha.
'Attoh ni rafiki yetu mkubwa sana na kila mara tulipokutana naye alikuwa na mke wake Maffiola. Yeye alikuwa akiupenda muziki huo wa hiphop, kitu kilichosababisha kujiunga na Hardcore Unity', alisema.

Kielimu, JCB anadai kumaliza shuli ya msingi mwaka 92 katika shule ya uhuru na sekondari ya Bondei. Baadae alianza kujiingiza katika masuala ya hiphop na kundi la HU squad na kuweza kupata deal kadhaa.

Wakati Spac Malic anasema alipata elimu ya msingi katika shule ya Meru na kufaulu kwenda Arusha secondary na kupata uhamishi kwenda Old Moshi ambapo alikataa kwenda shule, kwani aliona elimu aliyoipata primary ni ile same as ile ya sekondari.

Spac alisoma kozi mbalimbali ambazo ni lugha za Spanish, nyingine ni kozi ya wanyama kitu kitakachomfanya kuwafahamu wanyama na shughuli za kitalii hivyo kupata kipato kizuri.
JCB ambaye ni mchanganyiko wa Msukuma na Mnyivamba, wakati Spac anatoka Arusha.

Kuhusu producer wanayemuona ni mzuri sana ni Bonnie Luv ambaye pia ni DJ 88.4 Clouds FM. Hata hivyo Spac & JCB wanasema Master J na P Funk ni wazuri pia. Kwa upande wa group wanalolipenda ni Gangwe Mob ambao wamekuwa pamoja mara nyingi hapa Dar es Salaam.




:: OUR TZ HIP HOP ::
Crews A-Z
Weekly top 10
East African Updates Archive
Top 10 Audio Archive
Update (99)
Update (98)
Producers (97)
Bantu Pound
Underground Souls
Dola Soul
High V
E Attack

:: SWAHILI ::
Hardblasters Crew
Hardcore Unit

:: VIDEO ::
Hali Halisi

:: INTERVIEWS ::
Soggy Doggy
Bugsy Malone
Bonnie Luv
Hashim
Mack-D
Master J
Sos-B