Angola
Algeria
Benin
Botswana
Cameroon
Cabo Verde
Congo
Gambia
Ghana
Guinee
Ivory Coast
Kenya
Liberia
Madagascar
Malawi
Mali
Mozambique
Namibia
Nigeria
Rwanda
Senegal
South Africa
Swaziland
Tanzania
Togo
Uganda
Zambia
Zimbabwe



Hardblasters Crew wanaendelea kazi

Kikundi cha Hardblasters kimejulikana Bongo kwa muda mrefu. Mwaka huu wa 2000 kimezidi kupendwa kutokana na albam yao 'Funga kazi' na hit single 'Chemsha Bongo' & 'Mamsap'. Mwandishi wetu Eric Toroka amepata kuonana nao wale marepa maarufu na kujua historia ya kundi lao.



Kilianzishwa mwaka 1989, kikiwa na maana ya walipuaji au wapasuaji au wachangamzi wa vitu vigumu (mambo mazito) kikiwa na wasanii watano ambao ni:

William Shundi (Crazy One aka Simba)
Ngida Raphael (KC1)
Frank Kpyrassa (Trigger F)
Gabriel kilunga (Tuff Jam)
Terry Msiagi (Luni T aka Fanani)

Makazi au makao makuu yapo Upanga mashariki Dar es Salaam

Mnamo katikatik ya mwaka 1994 tulifanikiwa kutoa santuri yetu ya kwanza iliyojulikana kama Mambo ya mjini.
Ilitayarishwa na kurekodiwa katika studio za Mawingu chini ya msimamizi ya Clouds ent. Santuri hiyo ilikuwa na nyimbo nane ambazo ni Mambo ya mjini, Tupendane, Kua ukomae, Africa, Matapeli, Mabishoo, Ni Hardblasters na Nimeamini.

Mwaka huo huo 1994 mwishoni tukiwa tumeshaanza matayarisho ya santuri ya pili, huku tukisubiri mashindano ya rap ya taifa tulipata pigo la kutengana na mwenzetu Gabriel Kilunga (Tuff Jam) masomoni nchini Marekani. Hata hivyo pamoja na pigo hilo tulifanikiwa kushika nafasi ya pili tukiwa nyuma ya Kwanza Unit.

Mwaka uliofuata 1995 mwanzoni tulitumia kwa kumalizia hatua ya kwanza ya santuri yetu ya pili iliyojulikana kwa jina la 'Blast Enough' (mchanganuo wa kutosha) kwa kurekodi takriban nyimbo sita katika studio za Sound Crafters kisha kusimamisha zoezi la kurekodi kutokana na mitihani iliyokuwa ikiwakabili baadhi ya wenzetu ambao walikuwa bado wanafunzi.

Mwaka huo huo 1995 mwishoni tulishiriki mashindano ya rap ya taifa, na kufanikiwa kuchukua ubingwa. Na katika raundi ya kwanza ya mashindano hayo kwa mara ya kwanza tulipanda na aliyekuwa mfurukutwa namba moja wa Hardblasters bwana Jose Haule aka Nigga J aka Mti mkavu.

Mwaka uliofuata 1996 tuliendelea na kazi ya kurekodi santuri ya pili ambayo tuliimaliza katikati ya mwaka 1996. Santuri hiyo ina nyimbo kumi na nne ambazo ni
Upande a: Blast nuff, Wanikacha, Lunitech, Jaribu, Bust the rhyme, Bado moto na What's on. Upande B twapendeza, straight up. Aje nau?, Chana, Cheka nao, Boom check it out & Outro.

Na katika santuri kuna wasanii tuliowaalika ambao ni Trigga J, Killa B na Mkereketwa Nigga J.
Santuri yote imerekodiwa katika studio za Sound Crafters chini ya uhandishi wa Jason Figueiredo na Marlon Linje na Hardblasters wakiwa maproducer wahusika.
Mwaka huo huo mwishoni tukapata pigo jingine ambapo wasanii wenzetu wawili Ngida Raphael na Frank Korrassa waliamua kuachana na shughuli za kimuziki kutokana na na kukabliwa na masomo hivyo kufanya idadi yetu kupungua kutoka watano hadi wawili. Hali hii ilimlazimisha mkereketwa Nigga J kuwa mmoja wa Hardblasters kwa muda wote.
Mwaka uliofuata wa 1997 tulitumia kwa kufanya ziara nyingi za mikoani. Katika kutengeneza albam hii tukifika Morogoro, Dodoma, Mwanza n.k.
Mwaka huo huo tulijari kwa hali na mali kutafuta soko la kazi yetu kwa bei nzuri pasipo mafanikio hivyo kutufanya tutegemee live show zaidi kuliko mauzo ya santuri.

Mwaka huo huo tena tukafuatwa na FM bank ambaye baada ya kusikiliza kazi zikafanywa taratibu zote za uzinduzi ikiwa panoja na mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Peacock hotel, lakini cha kushangaza zoezi la uzinduzi likasimamishwa bila sababu yoyote hivyo kutufanya tuvunje mkataba na FM.

Mwaka 1998 ulikuwa tofauti na miaka mingine kwani mbali na kufanya ziara zaidi tulikuwa tukiandaa santuri ambayo ilikuwa na utazamo wa millenia mpya. Kwa mara ya kwanza tukiwa na producer wa kudumu Ludigo (Ludi) tuliweza kuandaa miendo mbinu ya kimuziki ya muda mrefu ambayo matokeo ni albam 'Funga kazi'.

Mwaka uliofuata wa 1999 tulirekodi nyimbo mbili katika studio ya Don Bosco, moja Mawingu Studio na nyimbo moja katika studio ya Master Jay.
Nyimbo hizo ni Pata pata, Soul Train, Kwenye rap na Chuzi limekubali ikiwa ni pasha moto ya santuri.

Mwaka uliofuata (millenia mpya) mwanzoni mwezi wa tatu tuliingia mkataba na studio za MJ production za Masaki jijini kurekodi santuri yetu ya tatu ilijulikana kwa jina la Funga Kazi yenye nyimbo 14 ambazo ni Funga Kazi, Chuzi limekubali, Chemsha Bongo, Eeh Mola, Mamsap, Pata potea, It's time 4 action (feat Killa B), Soultrain, Nakuzingua, Kwenye rap (feat Jeff Jafari & Total Maniac), 1/2 peponi 1/2 kuzimu (feat Jeff Jafari wa Gang Ghostkillaz), Tuko nyuma (feat LB Gervous), Kubwa kuliko (feat Mr Teacher), na Fanani. Nyimbo zote zimetengenezwa chini ya usimamizi wa Ludigo na Master J.


(c) 2000 Dar es Salaam. Imeandikwa na Eric Toroka - Africanhiphop.com (based on a biography by Hardblasters)




:: OUR TZ HIP HOP ::
Crews A-Z
Weekly top 10
East African Updates Archive
Top 10 Audio Archive
Update (99)
Update (98)
Producers (97)
Bantu Pound
Underground Souls
Dola Soul
High V
E Attack

:: SWAHILI ::
Hardblasters Crew
Hardcore Unit

:: VIDEO ::
Hali Halisi

:: INTERVIEWS ::
Soggy Doggy
Bugsy Malone
Bonnie Luv
Hashim
Mack-D
Master J
Sos-B

:: HARDBLASTERS ::
Lyrics: Chemsha Bongo
Audio: Mamsap
Audio: Chemsha Bongo