|
|
Angola Algeria Benin Botswana Cameroon Cabo Verde Congo Gambia Ghana Guinee Ivory Coast Kenya Liberia Madagascar Malawi Mali Mozambique Namibia Nigeria Rwanda Senegal South Africa Swaziland Tanzania Togo Uganda Zambia Zimbabwe |
|
Best G Historia yake na maelezo kuhusu matatizo yaliyokabili wasanii nchini Tanzania Best G ni msanii wa musiki wa hip-hop rap. Alizaliwa mnamo mwaka 1976 - Songea. Jina la awali anatambulika kama "George Njogopa". Alianza kujishughulisha na muziki tangu akiwa bado kijana mdogo, wakati huo alianza na kucheza disco "Night disco". Azma yake ya kuwa msanii wa musiki wa rap ilianza kujitokeza mara tu alipoanza elimu ya sekondary. Hapo ndipo alipoweza kukuta na marafiki na wakaanza kushauriana kuhusu musiki. Rafiki yake mkubwa alikuwa "Chriss Boy" ambaye baada ya masomo yao ya sekondary waliamua kundi lililojulikana kama "Black Youth Nature" ambalo liliwajumuisha wasanii wanne "Big Pac', "Prince Cool", "Best G" mwenyewe na rafiki "Chriss Boy" kundi hili lilikuwa tayari limeandaa single kama "Tanzania", "Kujichubua", "Janga la kuzimu" lakini halikuweza kurekodi kutokana na kutoelewana na baadaye likasambaratika. Hapo ndipo msanii Best G alipoanza shughuli zake mwenyewe kama msanii anayejitegemea "Solo artist", hata hivyo hakuwa za kupata mafanikio ya moja kwa moja kutokana na mazingira aliyokuwa akikabiliwa nayo. Best G, kama ilvyo wasanii wengine huimba musiki wa rap za Kiswahili na Kingereza. Tayari yuko mbioni kutoa "single" yake yenye nyimbo kama "DSM big city", "My secrety", "Mpenzi" ambazo zinategemea kutoka hivi punde. Matatizo ambayo yanatukabili wengi wetu ni kukosa mapromota pamoja na studio za kisasa za kuweza kurekodi na kuzitangaza kazi zetu na kama tunanufaika ni kwa kutegemea katika matamasha tu "concert" na hupeleka kutotambulika na kukosa mauzo ya album zetu. Vilevile tatizo la kipesa kwa wasanii wachanga limekuwa likikwamisha sana maendeleo ya kazi yetu. Ili uweze kukufanya recording na kuitangaza kazi yako na hata pia kuandaa ziara ya kutembelea baadhi ya maeneo kwa ajiri ya maonyesho ni lazima uwe na pesa za kutosha au ubahatike kupata mdhamini ambaye atakugharamia ili uweze kupata wapenzi wengi na hatimaye kupata mauzo mazuri ya "album" yako. Kutokuwa na ushirikiano dhabiti na vyombo vya habari ambavyo vinaweza kutumika kama promotion kwetu na kuwafanya wasanii wa changa wapate kutambulika na kuheshimika popote duniani kama vile magazeti, majarida, FM-radio, TV, vinatosha kabisa kumejenga na kumkubarisha msanii mbele ya watu na ukawa na maendeleo mazuri katika kazi yako. Best G c/o George Njogopa PO Box 14510 Dar es Salaam Tanzania |
|
|
|